WATAALAMU WA KILIMO WACHAMBUA BAJETI
Chama cha wataalamu wa uchumi wa kilimo nchini kimepongeza makadirio ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/2022. Akizungumza kwenye mkutano wa wataalamu hao uliofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Katibu wa chama hicho, Dr. Felix Nandonde kutoka Shule kuu ya Uchumi Kilimo (COEBS), alisema pamoja na mipango mizuri iliyopo kwenye bajeti hiyo, wameona yapo baadhi ya mambo yanapaswa kuongezwa na kuwekewa mkazo. Pia Profesor Khamaldin Mutabazi kutoka COEBS, alisema uchumi wa nchi unategemea kilimo na kwa kuwa na dira ya maendeleo ya nchi ya 2020/25 inakwenda kwenye uchumi wa viwanda, lazima sekta ya kilimo iwekewe mikakati.
Bofya hapa kwa habari kamili: Uchambuzi wa bajeti 2021/22 Uchumi wa kilimo