Sekta binafsi na za umma zimeshauriwa kuongeza uwekezaji kwenye zao la Kahawa kutokana na umuhimu wa zao hilo na fursa za kiuchumi kwenye maeneo ya kilimo cha kahawa nchini.
Kiongozi wa Mradi wa TRADE HUB Prof. Reuben Kadigi akizungumza na wadau kuhusiana na malengo ya mradi katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya utafiti
Hayo yamesemwa mnamo tarehe 1 Juni 2022 na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Joseph Rajabu Kangile alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti wa awali juu ya kutambua faida za kiuchumi, kijamii na kimazingira zitokanazo na biashara ya kahawa Tanzania, Jijini Dodoma. Utafiti huo ulilenga kuongeza uelewa kwa ajili ya kuchangia katika uundaji wa sera zitakazochochea biashara ya kahawa inayolimwa kwa uendelevu, usawa wa kijamii na uendelevu wa jumla katika mnyororo wa usambazaji Kahawa
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Joseph Rajabu Kangile akiwasilisha matokeo ya utafiti