Mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo Mh. Prof. Adoph Mkenda akizindua Kizimba Business Model (KBM) – SUGECO – Sokoine University of Agriculture Morogoro .
Mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo Mh. Prof. Adoph Mkenda akizindua Kizimba Business Model (KBM) mfumo wa kijasiriamali ulioanzishwa na SUGECO Kwa maendeleo ya kilimo nchini.
Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda alizindua mfumo wa Kizimba kuvutia vijana katika kilimo biashara tarehe 16 Machi 2021 SUGECO ikishirikiana na COEBS – Sokoine University of Agriculture (SUA)
Prof. Mkenda alipongeza mfumo huo na kusema “mfumo wa Kizimba utawezesha vijana wengi kujiunga pamoja kama ushirika na kutumia ardhi kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo kwa usimamizi wa wataalam wa taasisi hiyo”.
Pia amezitaka taasisi za kifedha nchini kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwavutia vijana wengi kujikita katika kilimobiashara kupitia mfumo wa Kizimba ‘Business Model’ unaoratibiwa na Taasisi ya SUGECO.
“Wito wa serikali kwa taasisi za kifedha hapa nchini nikutoa mikopo yenye riba nafuu ili waweze kuanzisha shughuli za kilimo kupitia mfumo huu wa kizimba ambapo utasaidia kuongeza tija na uzalishaji mazao ya kilimo hali itakayochochea ukuaji wa ajira na kuongeza kipato kwa vijana ” alisema Waziri Mkenda.
Ili kukuza tija na uzalishaji kwenye sekta ya kilimo Prof. Mkenda amesema wizara yake itaendelea kuhamasisha kujengwa kwa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo bora na huduma za ugani hatua itakayokuza tija kwenye kilimo.
Aliongeza kusema kuwa taasisi ya SUGECO inayoundwa na wahitimu inafanya kazi nzuri ya kuwaunganisha vijana wanaofanya kazi za kilimo kwa kuwapatia mafunzo kwa vitendo na kuwaunganisha na masoko.
“Sekta ya kilimo kinachangia chini ya theluthi moja kwenye pato la taifa (28%) na kwa upande wa kilimo mazao bado mchango wake ni chini na takribani theluthi mbili ya nguvu kazi ya watanzania inajishughulisha na kilimo hivyo tafsiri yake ni kuwa tija yetu bado ipo chini”
Tunataka tuongeze tija ili kilimo kichangie zaidi kwenye ukuaji wa uchumi” alisisitiza Prof.Mkenda
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Sokoine Prof.Raphael Chibunda alisema chuo hicho kitaendelea kushirikiana na wizara ya kilimo kusukuma na kubadilisha mfumo wa kilimo kuwa wa kibiashara ambapo sasa kimefanikiwa kuanzisha mashamba biashara kwenye maeneo yote ya chuo.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda akitoa ujumbe kwa wakati wa uzinduzi wa Kizimba Business Model
Mwenyekiti wa SUGECO Dr Anna Temu akielezea na kuonesha kwa mgeni rasmi na Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Sokoine Prof.Raphael Chibunda pamoja na wageni wengine vitu ambavyo vinazalishwa na kufanywa na SUGECO
Mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo Mh. Prof. Adoph Mkenda akiambatana na mkurugenzi wa SUGECO Revocatus Kimario, pamoja na wageni wengine wakitembelea mashamba ya mfano hapa SUGECO na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Ni katika uzinduzi wa mfumo wa kijasiriamali wa Kilimo cha kisasa cha mashamba makubwa ujulikanao kama KIZIMBA BUSINESS MODEL (KBM)
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini tukio la uzinduzi wa Kizimba Business Model (KBM) lililofanyika katika viwanja vya SUGECO Morogoro.
Mwenyekiti wa SUGECO Dr.Anna Temu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na wageni waliohudhuria tukio hilo